Siku ya Kimataifa ya Kujitolea: Ulimwengu wenye watu wanaojitolea bilioni nane

Zaidi ya watu bilioni moja wanaojitolea ulimwenguni kote wanafanya kwa umoja na ubinadamu kwa ajili ya watu na sayari. IVD ni siku ya kuwashukuru watu wanaojitolea ulimwenguni kote na kutambua thamani ya kazi za kujitolea katika amani na maendeleo.

Kauli mbiu ya IVD mwaka huu imejikita kwenye nguvu ya kila mmoja – kitendo cha pamoja – ikiwa kila mmoja akifanya. Ikiwa kila mmoja akijitolea ulimwengu ungekuwa sehemu bora. Fikiria zaidi ya watu bilioni nane kati yetu wanajitolea. Uwezekano usiyo na kikomo kwa maendeleo endelevu – chakula na elimu kwa kila mmoja, mazingira safi na afya nzuri, jamii jumuishi na zenye amani, na zaidi.

Kadri ulimwengu unavyokusanya nguvu kupambana na changamoto zinazoongezeka, ni watu wanaojitolea ndio wa kwanza kusaidia. Watu wanaojitolea ndio wapo mbele katika majanga na dharura, mara nyingi katika hali za majaribu na za kutisha.

“Kwenye siku hii muhimu, hebu tujitoe tena kuhakikisha kwamba watu wote wanaweza kuazima nguvu zao kwenye kutengeneza baadaye bora kwa ajili ya watu wote na sayari tunayochangia. Hebu tusimame na watu wanaojitolea, kila mahali.” António Guterres, Katibu Mkuu, Umoja wa Mataifa.

Shughuli za IVD zinaendelea ulimwenguni kote ikihusisha matukio makubwa saba yanayoadhimishwa na Serikali katika nchi za Azerbaijan, Bolivia, Iraq, Ireland, Tanzania, Thailand, na Togo.

Kutoka msafara wa kitaifa wa kujitolea nchini Togo hadi kwenye shughuli za kupanda miti kutambua tabia nchi nchini Azerbaijan hadi kwenye safari ya viti vya magurudumu vya watu wenye ulemavu wanaojitolea nchini Thailand – kila tukio linakuza uanuwai wa kujitolea ulimwenguni kote.

Nchi na makundi ya wanaojitolea wataonyesha roho ya kujitolea pamoja na jamii, wanataaluma, mashirika yanayojihusisha na kujitolea, na mawakala wa UN. Wafanyakazi wa UNV kwenye Makao Makuu jijini Bonn pia watashiriki katika shughuli ya kujitolea kuadhimisha IVD na kuonyesha roho ya kujitolea miongoni mwa wakazi wenyeji.

Leo ninasema kwa watu wanaojitolea wote ulimwenguni kote: Asante. Kwa kuchagua kuboresha ulimwengu. Kwa kupata hamasa ya kufanya. Kwa kutengeneza suluhisho. Kwa kuweka matumaini yetu hai. Na kwa ulimwengu ujumbe wetu ni: Fikiria tungefanikisha nini ikiwa wote wangejiunga. Na kujitolea.” Toily Kurbanov, Mratibu Mkuu, United Nations Volunteers.

Kwa kupaza sauti ya umoja katika majanga na machafuko, tunamtakia kila mmoja amani kwenye IVD 2023

MAELEZO YA MHARIRI:

Programu ya United Nations Volunteers (UNV) huwapa raia ulimwenguni kote fursa ya kujitolea kwenye nguzo zote tatu za mfumo wa Umoja wa Mataifa: maendeleo; amani na usalama; na haki za binadamu.

Ikiongozwa na Programu ya Maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UNDP), UNV inatetea utambuzi wa watu wanaojitolea, hufanya kazi na washirika kufungamanisha kazi za kujitolea katika programu za maendeleo, na kusaidia kuhamasisha watu wanaojitolea ulimwenguni kote.

UNV inafanya kazi katika nchi 160 ulimwenguni kote na inawakilisha utaifa wa nchi zaidi ya 170.

Siku ya Kimataifa ya Kujitolea (IVD), tarehe 5 Desemba, ilianzishwa na UN mnamo mwaka 1985 kama adhimisho la kimataifa kusherehekea nguvu na uwezo wa kazi za kujitolea.

Ungana nasi katika kuwatambua watu wanaojitolea ulimwenguni kote kupitia kampeni yetu kwenye mitandao ya kijamii: #IfEveryoneDid #IVD2023

Bofya kutazama vyanzo vyetu vya IVD: Webpage | Trello | Promo Materials

Taarifa za Mawasiliano:

Jennifer Stapper

Communications Global Team Lead

External Relations and Communications Section United Nations Volunteers [email protected]

www.unv.org

MWISHO